Je wajumbe wanaweza kumpokonya Trump ushindi?

Jopo la kumchagua rais nchini Marekani linakutana Jumatatu kuamua nani atakayeongoza Marekani
Image caption Jopo la kumchagua rais nchini Marekani linakutana Jumatatu kuamua nani atakayeongoza Marekani
  • Jopo la kumchagua rais hufanya kazi vipi?

Wanachama 538 wa jopo la kumchagua rais nchini Marekani wanakutana Jumatatu katika miji mkuu ya majimbo yote hamsini ili kumteua atakayemrithi rais Barack Obama kama rais wa Marekani.

Mgombea ni sharti apate wingi wa kura hiyo ya wajumbe ama kura 270 za wajumbe 538 ili kushinda urais.

  • Kwa nini Jopo la kuchagua rais?

Mfumo huo ulianzishwa na katiba ya Marekani mwaka 1787. Katiba imeweka sheria hiyo ya kupiga kura ya urais isio moja kwa moja ambapo wanawake na wanaume hawakuruhusiwa kupiga kura wakati huo.

Waanzilishi wa taifa hilo waliiweka sheria hiyo kama maafikiano kati ya kura ya rais inayopigwa moja kwa moja ambapo kila raia anaruhusiwa kushiriki na uchaguzi unaohusisha wabunge hatua iliokataliwa kwa kuwa haina demokrasia.

Tangu wakati huo kumekuwa na mapendekezo mengi ya marekebisho ya kikatiba kwa lengo la kuliondoa jopo la kumchagua rais, lakini hakuna mtu aliyefaulu.

  • Ni akina nani wanaomchagua rais?

Kuna takriban wajumbe 538.Wengi wao ni maafisa waliochaguliwa au viongozi wa vyama, lakini majina yao hayapo katika makaratasi ya kupigia kura na pia hawajulikani na umma.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Baadhi ya raia wanaopinga maamuzi wa jopo la kumchagua rais nchini Marekani

Kila jimbo lina wajumbe wengi kwa kuwa lina wabunge katika bunge la uwakilishi {Idadi yao inategemea idadi ya watu katika jimbo hilo na katika bunge la seneti kuna wawili kila jimbo licha ya ukubwa wa eneo.}

Jimbo la California lililo na idadi kubwa ya watu lina wajumbe 55, Texas lina 38 huku majimbo yalio na idadi ndogo ya watu kama vile Vermont ,Alaska,Wyoming na Delaware yana wajumbe watatu kila mmoja pamoja na District of Colombia.

Katiba inayapa nguvu majimbo kuamua vile wajumbe wake watakavyopiga kura.

Katika kila jimbo isipokuwa Nebraska na Maine, mgombea anayeshinda wingi wa kura ndio mshindi wa wajumbe wa jimbo hilo.

  • Kwa nini wajumbe wanaangaziwa sana mwaka huu?

Katika uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Novemba ,Donald Trump alishinda kwa wingi wa wajumbe 306 kati ya 538, lakini mpinzani wake wa chama cha Democrat alishinda kura nyingi za kawaida na kumshinda Trump kwa takriban kura milioni 3.

Image caption Aliyekuwa mgombea wa chama cha Democrat Hillary Clinton na rais mteule wa Marekani Donald Trump

Ijapokuwa hali hiyo ni ya kawaida nchini Marekani kufuatia matokeo kama hayo mwaka 2000 ambapo George Bush alimshinda Al Gore, matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu uliojaa wasiwasi yaliwashangaza wengi.

Mamilioni ya raia wa Marekani ambao wanamuona Donald Trump kama asiyeweza kuongoza Marekani, wametia sahihi ombi katika mtandao wakiwataka wajumbe wa Republican kuzuia uchaguzi wake.

Wajumbe 37 watalazimika kufanya hivyo ili kumzuia kuchaguliwa kuwa rais.

Kambi ya Republican imepinga hatua hiyo ikisema ni jaribio la wanachama wa Democrat wasiotaka kukubali kushindwa na imelalamika kwamba baadhi ya wajumbe wamenyanyaswa kufuatia kura hiyo muhimu.

  • Je, ni kura ilio na muhimu ama ni ya kumuidhinisha aliyechaguliwa tu?

Hakuna sheria katika katiba ama hata katika sheria ya kijimbo inayowaruhusu wajumbe kumpigia kura mtu fulani.

Sheria katika majimbo mengine inawaruhusu wajumbe kuheshimu kura ya kawaida na wajumbe wanaokaidi amri hiyo hupigwa faini, huku majimbo mengi yakiwa hayana faini yoyote inayotolewa.

Historia inaonyesha kwamba sio jambo la kawaida kwa mjumbe kukaidi matakwa ya wapiga kura wa jimbo lake

Image caption Jopo la kumchagua rais nchini Marekani

Huku baadhi wakiwa wameenda kinyume na matakwa hayo, hawajaweza kubadili msimamo wao kuhusu mtu atakayechukua ikulu ya White House kwa muhula wa miaka minne.

  • Je ni lini matokeo ya uchaguzi yatatangazwa?

Huku wanachama wa jopo la kumchagua rais wakipiga kura siku ya Jumatatu, majimbo yana hadi Disemba 28 kutoa cheti chao cha kura kwa bunge la Congress pamoja na Makavazi ya kimataifa mjini Washinton, ambayo yataweka matokeo hayo mtandaoni.

Tangazo rasmi la rais aliyechaguliwa litatolewa na bunge la Congress mnamo tarehe 6 mwezi Januari.