Maandamano ya kumtaka Kabila kujiuzulu yafanyika duniani

Maandamano ya kumtaka kabila kuondoka madarakani yafanyika duniani Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maandamano ya kumtaka kabila kuondoka madarakani yafanyika duniani

Kumekuwa na maandamano katika miji kadhaa mikuu duniani ya kumtaka rais wa DR Congo Joseph Kabila kujiuzulu.

Leo ni siku ya mwisho ya utawala wake ,lakini uchaguzi umeahirishwa ambapo upinzani wa taifa hilo unasema kuwa ni jaribio la Kabila kusalia madarakani.

Image caption Vikosi vya usalama vikipiga doria katika mji wa kinshasa nchini DR Congo

Katika mji mkuu wa Kinshasa na kwengineko, kuna idadi kubwa ya vikosi vya usalama na raia wameamua kusalia majumbani mwao.

Takriban watu 40 wamekamatwa katika mji wa mashariki wa Goma.

Mazungumzo na upinzani yanayofanywa na viongozi wa makanisa yamefeli kuafikia mwafaka, jaribio jingine la kuendeleza mazungumzo hayo litaendelea siku ya Jumatano.

Image caption Mji wa Kinshasa nchini DR Congo

Zaidi ya watu hamsini walifariki katika makabiliano ya barabarani mnamo mwezi Septemba.