Balozi wa Urusi apigwa risasi na kufariki Uturuki

Mtu aliyempiga risasi balozi huyo wa Urusi alitoa ujumbe kuhusu mji wa Aleppo nchini Syria Haki miliki ya picha AP
Image caption Mtu aliyempiga risasi balozi huyo wa Urusi alitoa ujumbe kuhusu mji wa Aleppo nchini Syria

Balozi wa Urusi aliyepigwa risasi nchini Uturuki Andrey Karlov amefariki.

Balozi huyo alishambuliwa katika eneo la sanaa ya uchoraji katika mji mkuu wa Ankara.

Ripoti zinasema kuwa balozi huyo alikuwa akitoa hotuba wakati mtu aliyekuwa amejihami na bunduki alipompiga risasi na kutoa ujumbe kuhusu mji wa Aleppo nchini Syria.

Watu kadhaa wamejeruhiwa .Picha za tukio hilo zimewaonyesha watu wawili waliovalia nadhifu wakilala ardhini ,karibu na kipaza sauti.

Uturuki na Urusi zimekuwa zikizozana kuhusu kujihusisha kwao nchini Syria.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Balozi wa Urusi aliyepigwa risasi nchini Uturuki alipokuwa akihutubia

Kumekuwa na maandamano nje ya ubalozi wa Urusi mjini Istanbul katika siku za hivi karibuni kuhusu hatua ya Urusi kuunga mkono serikali ya Syria.

Lakini serikali za Uturuki na Urusi zimekuwa zikishirikiana katika usitishwaji wa vita huko Aleppo.