Shughuli za uokoaji zaimarishwa Aleppo

Watoto wakifurahia kuondoka Mjini Aleppo
Image caption Watoto wakifurahia kuondoka Mjini Aleppo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekubaliana na maamuzi ya kutaka kupelekwa kwa waangalizi wa Umoja wa Mataifa haraka huko Mashariki mwa Mji wa Aleppo ulioshikiliwa na waasi.

Baraza hilo litasimamia shughuli za uokoaji wa wahanga na wananchi kutoka eneo la mji huo, ambapo vikosi vinavyounga mkono serikali watatawala eneo hilo. Inaaminika kwamba watu elfu thelathini wanaweza wakajiunga na shughuli za uokoaji.

Watoa misaada wanasema kwamba karibia watoto hamsini waliokuwa wamekwama katika kituo cha kulelea yatima nao wameondolewa lakini wengi wao wamejeruhiwa vibaya wakati wa mapigano.