Leicester kukaa rufaa kadi nyekundu ya Vardy

Vardy Haki miliki ya picha Google
Image caption Mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy

Mabingwa watetezi wa ligi kuu England Leicester City wanapanga kukata rufaa kupinga kadi nyekundu aliyopewa mshambuliaji wake Jamie Vardy katika mchezo dhidi ya Stoke City.

Vardy alionyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi Craig Pawson, baada ya kumchezea rafu mshambuliaji wa Stoke Mame Diouf.

Leicester inataka kupeleka utetezi kwa chama cha soka England kuonyesha Vardy alisukumwa na hakuwa na nia ya kumfanyia rafu Mame Diof

FA inatarajiwa kuitoza faini Leicester baada ya wachezaji wake sita kuonyeshwa kadi za njano katika mchezo huo