Ujauzito hubadilisha ubongo wa mwanamke

Mwanamke mwenye mimba Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Kiwango cha homoni huongezeka sana mwanamke akiwa na mimba

Wanasayansi wanasema kuwa mjamzito hubadilisha ubongo wa mwanamke, kwa kipindi cha hadi miaka miwili.

Wanasema uja uzito hupunguza seli za ubongo katika baadhi ya sehemu za ubongo wa mwanamke, ili kumuwezesha kuhusiana vyema zaidi na mtoto na kujiandaa kwa majukumu yake kama mama.

Uchunguzi ulifanyiwa wanawake 25 waliokuwa wameshika mimba kwa mara ya kwanza ulionyesha mabadiliko hayo kwenye ubongo hudumu kwa hadi miaka miwili baada ya mwanamke kujifungua.

Watafti hao wanasema vipimo vya sehemu tofauti za ubongo hubadilika kipindi hicho, sawa na inavyofanyika mtu anapovunja ungo.

Lakini hata hivyo, hawakupata ushahidi wowote wa kuathirika kwa uwezo wa mwanamke kuweka kumbukumbu.

Watoto wasioweza kuugua Ukimwi

Majina mashuhuri zaidi ya watoto

Wanawake wengi husema huwa wanajihisi kuwa wasahaulivu na kuwa wepesi wa kuekwa na hisia wakati wanabeba mimba.

Mara nyingi huwa wanalaumu kilichobandikwa kuwa ubongo wa "uja uzito" au "mtoto".

Ongezeko la homoni

Mwanamke anapokuwa na mimba, kiwango cha homoni ya oestrogen huongezekana sana na pia mwili wake kubadilika, watafiti wanasema.

Hata hivyo, si wataalamu wengi walikuwa wamechunguza mabadiliko kwenye ubongo.

Watoto kuzaliwa na wazazi watatu Uingereza

Watafiti kutoka vyuo vikuu vya Universitat Autonoma de Barcelona na Leiden walichunguza ubongo wa wanawake kabla ya kushika mimba, muda mfupi baada ya kujifungua na miaka miwili baadaye kuangalia mabadiliko kwenye ubongo.

Matokeo ya utafiti wao yamechapishwa kwenye jarida la Nature Neuroscience.

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Mabadiliko hayo kwenye ubongo yanaaminika kuwaandaa wanawake kuwa na uhusiano mwema na watoto wao

Walilinganisha mabadiliko hao kwenye ubongo wa wanawake na ubongo wa wanaume 19 waliokuwa wamekuwa baba mara ya kwanza,wanaume 17 ambao hawakuwa na watoto na wanawake 20 ambao hawajawahi kujaliwa watoto.

Walishuhudia kupungua sana kwa seli za ubongo katika maeneo ambayo hutumiwa na ubongo katika kuhusiana na watu wengine.

Watafiti wanasema mabadiliko hayo huenda ni ya kuwafaa wanawake kwa njia kadhaa zikiwemo - kuwawezesha kupangia mahitaji ya watoto wao, kuwa na ufahamu zaidi kuhusu hatari kwa watoto wao kutoka kwa jamii na pia kuwawezesha kuhusiana zaidi na watoto wao.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii