Utafiti: Seli za maji maji ya uzazi huzuia mtu kuzeeka

Picha ya mifupa Haki miliki ya picha SPL
Image caption Picha ya mifupa

Seli katika maji ya uzazi yanayozuia mtoto katika tumbo la mama mjamzito huzuia mtu kuwa mzee kwa haraka mbali na kuimarisha mifupa kulingana na wanasayansi wa Uingereza.

Ugunduzi huo utasaidia watoto wenye magonjwa ya jeni ,watu wazee na hata wanaanga, kulingana na wanasayansi hao.

Ugunduzi huo katika panya uliochapishwa katika ripoti za kisayansi ,unaonyesha kuwa seli katika maji hayo ya uzazi huimarisha mifupa na kupunguza pakubwa uwezekano wa mifupa hiyo kuvunjika kwa asilimia 80.

Majaribio ya ugunduzi huo miongoni mwa binaadamu yataanza katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Maji hayo ya uzazi ndio yanayomlinda mtoto dhidi ya mtikiso wowote kutoka nje.Watafiti hao walikusanya seli hizo za maji ya uzazi kabla ya mtoto kuzaliwa.

Kundi hilo la wanasayansi kutoka chuo kikuu cha taasisi ya afya ya watoto ikishirikiana na chuo kikuu cha London ,kiliwadunga panya wagoinjwa seli hizo.

Haki miliki ya picha SPL
Image caption Picha ya sindano iliodungwa katika maji ya uzazi

Wanyama hao walikuwa na ugonjwa wa mifupa.

Miongoni mwa binadamu ,hali hiyo huathiri mtu mmoja kati ya 25,000 wanaozaliwa na inaweza kusababisha kifo mbali na watoto waliozaliwa na mifupa inayoweza kuvunjika.

Hata wale walionusurika hukabiliwa na hatari ya kuvunjika mifupa mara 15 kwa mwaka, meno yanayoweza kuvunjika kutoweza kusikia pamoja na ukuwaji.

Mifupa ya panya waliodungwa seli hizo baadaye iliimarika na kuwa na nguvu kama wanayama wengine.kiwango cha kuvunjika kwa mifupa hiyo kilishuka