Watu ishirini wauawa nchini DRC

DRC
Image caption Joseph Kabila Rais aliyemaliza muda wake

Umoja wa mataifa umeeleza kuwa watu zaidi ya ishirini wameuawa katika maandamano yaliyojiri katika miji kadhaa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo dhidi ya Rais Joseph Kabila.

Majeshi nchini humo inaarifiwa walitumia risasi za moto kuwashambulia waandamanaji katika mji mkuu wa Kinshasa, ambako watu walifunga barabara huku wakichoma matairi chakavu ya magari.

Milio ya risasi ilisikika pia katika mji mweingine wa pili kwa ukubwa ,lubumbashi, na taarifa zinaeleza pia kwamba askari polisi wawili wamepoteza maisha katika sintofahamu hiyo.

Maandamano hayo yana lengo la kumshinikiza rais aliyemaliza muda wake , Joseph Kabila kuachilia madaraka kufuatia muhula wake kufikia tamati mwanzoni mwa wiki hii.

Uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umeahirishwa mpaka mwak wa 2018 kutokana na hali tete ya kisiasa na ukosefu wa amani kutanda nchini humo.