Vardy kukosa mechi tatu za Epl

Jamie Vardy Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jamie Vardy

Mshambuliaji wa timu ya Leicester City Jamie Vardy atakosa michezo mitatu ya ligi kuu England baada ya Fa kutupilia mbali rufaa iliyokatwa na Leicester City.

Vardy alitolewa nje kwa kuonyeshwa nyekundu katika mchezo wa ligi kuu England baada ya kumchezea vibaya Mame Diouf.

Michezo atakayoikosa mchezaji huyu ni dhidi ya Everton mchezo wataocheza ugenini kwenye uwanja wa Goodson Park,kisha atakosa mchezo na West Ham utaochezwa King Power.

Vard pia atakosa mchezo wa Januari 2 dhidi Middlesbrough, hata hivyo mshambuliaji huyu atareje dimbani januari 7 mwakani, katika mchezo wa raundi ya tatu ya kombe la FA, ambapo timu yake itacheza na Everton