Mlipuko wauwa watu 26 Mexico

Mexico Haki miliki ya picha MEXICAN RED CROSS/ TWITTER
Image caption Picha ya mtandao wa Twitter ikionyesha eneo la soko kulipotokea mlipuko

Takribani watu 26 wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa kutokana na mlipuko mkubwa wa moto uliotokea katika soko la fataki San Pablito kilomita 36 nje kidogo ya mji wa Mexico city.

Wingu zito la moto kutokana na mlipuko huo katika soko la fataki la San Pabito,Umesababisha watu kuchanganyikiwa na kukimbia huku na kule kwa lengo la kujiokoa.

Picha za video zilizorushwa katika televishen nchini humo zimeonyesha anga la soko hilo likiwa limeunikiwa na wingu refu la moto.

Makundi ya uokoaji yamefika katika eneo la tukio kutoa msaada,na watu wametahadhalishwa kutosogea katika eneo hilo na barabara kuachwa wazi.

Gavana wa eneo hilo Eruviel Avila amesema kuwa kwa sasa nguvu kubwa imeelekezwa kusaiia majeruhi na watoa huduma wa serikali wamepelekwa katika eneo hilo

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa idadi ya milipuko iliendelea ada ya mlipuko wa kwanza na hatimaye oshi mkubwa na moto ukafunika anga.

Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto,kupitia ukurasa wake wa weeter ametoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao kutokana na mlipuko huo na majeruhi

Soko hilo la fataki la San Pablito mwaka 2005 lilikumbwa kasa kama huo,pale mfulilizo wa milipuko na moto mkubwa ulipozuka wakati taifa ilo liijiandaa kwa sherehe za uhuru.