Hali ya utulivu yerejea nchini DR Congo

Hali ya utulivu yarejea nchini DR Congo
Image caption Hali ya utulivu yarejea nchini DR Congo

Hali ya utulivu imerejea katika barabara za mji mkuu wa Kinshasa pamoja na zile za miji mingine muhimu nchini DR Congo kufuatia maandamano.

Kiongozi wa upinzini nchini humo Etienne Tshisekedi , amewataka wafuasi wake kuipinga serikali ya rais Joseph Kabila .

Kundi la upinzani lamtaka Kabila kujiuzulu

Maandamano ya kumtaka Kabila kujiuzulu yafanyika duniani

Watu 20 wauawa katika maandamano DR Congo

Zaidi ya watu 20 wameuawa katika ghasia baada ya muhula wa Kabila kukamilika siku ya Jumatatu usiku huku uchaguzi ukiwa umeahirishwa hadi 2018.

Kanisa katoliki linatarajiwa kuendeleza mazungumzo kati ya upinzani na muungano wa kitaifa.

Image caption Maandamano ya kumpinga rais Kabila yalifanyika huku zaidi ya watu 20 wakidaiwa kuuawa na wanajeshi

Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa anasema kuwa kanisa linaheshimiwa sana nchini humo kwa miongo kadhaa na kwamba mazungumzo hayo huenda yakatuliza hali ya wasiwasi iliopo iwapo upinzani na serikali hawataafikiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii