Ethiopia yatangaza 'kuwaachilia mahabusu takriban 10,000'

Waandamanaji Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wengi miongoni mwa mahabusu hao wanatoka katika majimbo ya Oromia na Amhara,

Ethiopia inasema kuwa inawaachilia karibu watu 10,000 waliokuwa wamefungwa chini ya sheria ya hali ya tahadhari iliyowekwa na serikali ya nchi hiyo mwezi Oktoba.

Wengine 2,500 watashtakiwa kwa makosa ya uhalifu yaliyofanyika wakati wa maandamano.

Maafisa wanasema kuwa wale watakaoachiliwa watapewa mafunzo maalum kuhakikisha kwamba hawajihusishi tena katika "tabia za usumbufu".

Wengi miongoni mwa mahabusu hao wanatoka katika majimbo ya Oromia na Amhara, ambako kulikuwa na maandamano ya upinzani ya miezi kadhaa dhidi wakidai kudhulumiwa kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Hali kwa sasa imekuwa ya utulivu tangu kuanza kutekelezwa kwa hali ya tahadhari.