Jamii ya kimataifa yamtaka Kabila kujiuzulu

Rais Joseph Kabila wa DR Congo ametakiwa na jamii ta kimataifa kung'atuka mamlakani
Image caption Rais Joseph Kabila wa DR Congo ametakiwa na jamii ta kimataifa kung'atuka mamlakani

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila anazidi kupokea shinikizo kimataifa kutokana na hatua ya kukataa kuachia maamlaka baada ya muhula wake wa kikatiba kukamilika jumatatu.

Ufaransa imesema itatuma ombi kwa umoja wa ulaya la kumwekea vikwazo iwapo ataendelea kushikilia maamlaka.

Watu 20 wauawa katika maandamano DR Congo

Hali ya utulivu yerejea nchini DR Congo

Baraza jipya la mawaziri latangazwa DR Congo

Ujerumani imehairisha majadiliano ya kuipa DR Congo msaada wa miradi ya maendeleo.

Image caption Maafisa wa usalama wakikabiliana na maandamano nchini DR Congo

Inaripotiwa kwamba utulivu umerejea nchini humo baada ya kushuhudiwa machafuko Jumatano, ambapo kulingana na Umoja wa Mataifa, takriban watu 20 waliuwawa.

Uchaguzi mkuu ulioratibiwa kufanyika mwaka huu, uliharishwa hadi mwaka 2018

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii