Barcelona ,Sevilla zapeta Copa del Rey

Barcelona Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wachezaji wa Barcelona wakishangilia bao

Miamba wa Soka wa Hispania Barcelona waliibuka na ushindi wa kishindi wa mabao 7-0 dhidi ya Hercules katika michuano ya kombe la Mfalme maaarufu kama Copa del Rey.

Nao Sevilla wakaibuka na ushindi wa kishindo kwa kuichapa kwa mabao 9-1 timu ya SD Formentera , mshambulia Luciano Dario Vietto pamoja na Wissam Ben Yedder wote walifunga hatrick katika mchezo huo.

Eibar wao waliibuka na ushindi wa 3 - 1 Sporting Gijon, Deportivo La Coruna wakashinda kwa ushindi wa mabao 3 - 1 dhidi Real Betis.

Osasuna wakaibuka wababe kwa kuichapa Granada kwa 2 - 0 Valencia wakashinda kwa mabao 2 - 1 dhidi ya Leganes