Mwanaharakati anatuhumiwa kwa Rushwa

Waandamanaji walioshikilia mabango ya kumtaka milargo aachiwe.
Image caption Waandamanaji walioshikilia mabango ya kumtaka milargo aachiwe.

Polisi nchini Argentina wamepambana na waandamanaji waliokuwa wakuijaribu kuingia mahakamani ambapo mwanaharakati maarufu Milagro Sala anatuhumiwa kwa Rushwa. Watu tisa na polisi watatu wamejeruhiwa.

Baadhi ya wapinzani walikuwa ni wabunge wa vyama pinzani wanaolaumu polisi kwa vitendo vya kikatili.

Mwanaharakati huyu Milagro Sala ni mwenyeji wa Argentina na ni mwenyekiti wa kikundi kijulikanacho kama Tupac Amaru social welfare group, kinasambaza misaada ya kijamii kwa wananchi wanaoishi katika mazingira magumu kusini mwa jimbo la Jujul.

Mwanaharakati huyo amesema anatuhumiwa na mamlaka za serikali kwa maoni yake ya kisiasa