Kvitova kuwa nje ya uwanja kwa miezi sita

Petra Haki miliki ya picha Google
Image caption Petra Kvitova

Mshindi mara mbili wa michuano ya Wimbledon, mcheza tenesi Petra Kvitova,atakua nje ya uwanja kwa miezi sita baada ya kushambuliwa na kisu.

Kvitova mwenye umri wa miaka 26,alifanyiwa upasuaji wa mishipa katika kiganja cha mkopo anaotumia kuchezea tenesi.

Daktari aliyemfanyia upasuaji nyota huyo wa tenesi amesema itachukua miezi mitatu kuweza kuwa tayari tena kushika fimbo ya kuchezea tenesi.