Chama tawala chapitisha sheria ya uchaguzi Kenya

Bunge la Kenya
Image caption Bunge la Kenya

Chama tawala nchini Kenya, Jubilee kimefanikiwa kupitisha sheria tata itakayoruhusu utumizi wa mfumo wa kuhesabu kura kupitia mkono wakati wa uchaguzi ujao.

Mfumo huo utatumika iwapo mfumo wa kielektroniki utafeli katika maeneo ambayo hayana umeme ama hata mtandao.

Usajili wa wapiga kura, ukaguzi wa maswala yote ya shughuli hiyo wakati wa uchaguzi mbali na kusafirishwa kwa kura kutafanywa kwa njia ya mkono.

Wabunge wa serikali waliwashinda wenzao wa upinzani ambao waliweza kuzuia marekebisho hayo siku ya Jumanne.

Upinzani umekuwa ukipinga sheria hiyo ukisema inalenga kusababisha wizi wa kura kwa kutumia mfumo wa kielektroniki ili kusimamia usajili wa wapiga kura na utambuzi wa wapiga kura.

Viongozi wa upinzani wameenda mahakamni kupinga hatua hiyo.