Diafra Sakho kutocheza kwa wiki nane

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Diafra Sakho (kulia) ni mshambuliaji wa West Ham na Senegal

Mshambuliaji wa West Ham na Senegal Diafra Sakho hatashiriki katika mechi ya kuwania kombe la taifa bingwa barani Afrika baada ya kuripotiwa kuwa hatacheza kwa kipindi cha wiki nane zaidi kutokana na jeraha.

Klabu ya West Ham ilisema tarehe 30 mwezi Novemba kuwa mshambuliaji huyo wa umri wa miaka 26 hatacheza kwa wiki sita ikimaanisha kuwa hatarejea uwanjani hadi kati kati ya mwezi wa Januari.

Lakini meneja wa West Ham Slaven Bilic, amesema kuwa Sakho huenda asicheze kwa kipindi cha wiki nane na huenda sasa akarejea kati kati ya mwezi Februari.