Ndege iliyotekwa nyara nchini Libya yatua Malta

Ndege hiyo ilikuwa safarini ndani mwa Libya Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ndege hiyo ilikuwa safarini ndani mwa Libya

Ndege moja ya Libya iliyoripotiwa kutekwa nyara ikiwa kwenye safari ya ndani mwa nchi imetua nchini Malta.

Ndege hiyo aina ya Airbus A320 ya shirika la ndege la serikali ya Libya, Afriqiyah, ilikuwa na abiria 118 wakati ilitekwa.

Watekaji nyara wawili waliripotiwa kutishia kuilipua ndege hiyo.

Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka mji wa Sebha kusini magharibi mwa Libya ikielekea mji mkuu Tripoli kabla ya kuelekezwa nchini Malta, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Karibu watu wote waliokuwa ndani ya ndege wanaripotiwa kuondoka.

Watekaji nyara hao waliondoka ndani ya ndege hiyo na kujisalimisha.

Mmoja wao alikimbia kituo kimoja cha runinga nchini Libya kuwa yeye ni mkuu wa chama chama kinachompendelea kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi.

Meya wa mji wa Sebha nchini Libya ambapo ndege hiyo ilikuwa ikitokea anasema kuwa watekaji nyara hao wanatafuta hifadhi ya kisiasa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Vikosi maalum vya ulinzi vilionekana uwanjani
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Vikosi maalum vya ulinzi vilionekana uwanjani
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watekaji nyara wawili walitishia kuilipua ndege hiyo