Mwanamke "afufuka" India

Mwanamke huyo alifikiriwa kuada dunia miaka 40 iliyopita
Image caption Mwanamke huyo alifikiriwa kuada dunia miaka 40 iliyopita

Mwanamkee mmoja wa India aliyefikiriwa na familia yake kwamba alikufa miaka 40 iliyopita, ameshangaza watoto wake kwa kutokeza tena.

Kwa vile alifikiriwa amekufa baada ya kutafunwa na nyoka, Vilasa Devi hakuchomwa moto.

Aliachwa kueleea kwenye mto wa Ganges.

Sasa akiwa na umri wa miaka 80, aliiambia BBC kwamba aliokolewa na wavuvi, umbali wa mamia ya kilomita. Akapokelewa na familia moja.

Aliolewa, kwa vile alipoteza fahamu kwamba tayari aliwahi kuolewa na kwamba alikuwa na watoto.

Karibuni, kwa bahati, alikutana na mwanamke wa kijiji chake ambaye alimzindua.

Akarudi nyumbani, kama aliyefufuka. Waume zake wote watatu, wameshafariki.