Tunisia yamkamata mpwa wa mshambuliaji wa Berlin

IS walitoa kanda ya video ikimuonyesha Amri akilitii kundi hilo Haki miliki ya picha AFP
Image caption IS walitoa kanda ya video ikimuonyesha Amri akilitii kundi hilo

Vikosi vya usalama nchini Tunisia vimemkamata mpwa wa mshambuliaji kwenye soko mjini Berplin, Anis Amri na washukiw wengine wawili.

Wizara ya masuala ya ndani nchini Tunisia, inasema kuwa watu hao wenye umri kati ya miaka 18 na 27 ni wanachama cha kundi la kigaidi.

Mzaliwa wa Tunisia Amri, mwenye umri wa miaka 24, aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi karibu na mji wa Milan nchini Italia mapema Ijumaa.

Shambulizi la lori la siku ya Jumamosi kwenye soko, lilisababisha vifo vya watu 12 na kuwajeruhi wengine 49.

Wizara ya masuala ya ndania ilisema kuwa mpwake huyo Amri, alikiri kuwasiana na mjombake kupitia mtandoa wa Telegram ili kukwepa kuchunguzwa.

Inaripotiwa kuwa watatu hao wemekuwa wakihudumu kwenye miji ya Fouchana nje ya mji wa Tunis na Oueslatia karibu na nyumbani kwao Amri, umbali wa kilomita 150 kutoka mji mkuu.