Israel yawashtumu mabalozi wa UK, Urusi, China na Uhispania

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Image caption Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Waziri Mkuu wa Israil, Benjamin Netanyahu ameamrisha wizara ya mashauri ya nchi za nje, kuwaita na kuwaonya mabalozi wa nchi zinazowakilishwa katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Bwana Netanyahu amekasirishwa na hatua ya Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa kupiga kura ya kulaani ujenzi wa makaazi ya Wayahudi, katika ufukwe wa magharibi eneo la Wapalestina linalokaliwa na Israil.

Mabalozi wa Ufaransa, Uingereza, Urusi, Uchina na Uspania wote ni kati ya walioitwa.

Mwakilishi wa Marekani mjini Tel Aviv hatotakiwa kwenda serikalini.

Image caption Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na rasi Barrack Obama kulia

Kwa sababu Marekani haikutumia kura yake ya turufu, veto, ndio imewezesha azimio kuipitishwa.

Marekani haikupiga kura katika azimio hilo lakini piya halikuunga mkono.