Ndege ilioanguka: Rais Putin ataka uchunguzi Ufanywe

Rais Vladmir Putin wa Urusi
Image caption Rais Vladmir Putin wa Urusi

Rais Putin ameagiza uchunguzi ufanywe kuhusu ndege ya jeshi la Urusi, iliyoanguka katika Bahari ya Black Sea, punde baada ya kuondoka Sochi, ikielekea Syria.

Hakuna aliyenusurika kati ya watu zaidi ya 90 iliyobeba.

Televisheni ya Urusi imecheza rekodi ya mawasiliano ya mwisho baina ya wanaoongoza safari za ndege ardhini na rubani wa ndege hiyo.

Hapakuwa na ishara ya matatizo, na rubani alisikika ametulia, hadi ndege ilipotoweka.

Abiria wengi walikuwa kutoka kikundi cha bendi ya muziki cha jeshi kikundi cha Alexandrov Ensemble kilichopata sifa.