Kimbunga Nock Ten chapiga Ufilipino

Kimbunga Nock-Ten chakumba taifa la Ufilipino
Image caption Kimbunga Nock-Ten chakumba taifa la Ufilipino

Kimbunga kikali, kilichopewa jina la Nock-Ten, au Nina, kikivuma kwa kasi ya kilomita mia moja na thamanini natano, kinapiga Ufilipino.

Watu wanaoishi njia ya kimbunga hicho, wasiotaka kuondoka majumbani mwao wameamrishwa kuhama.

Maelfu wengine waliokuwa wakielekea makwao kwa Krismasi wamenaswa njiani, kwa sababu safari za ndege na za meli zimevunjwa.

Wakuu wameonya kwamba utatokea uharibifu wa majumba na mashamba.

Kimbunga hicho kinatarajiwa kupiga eneo lenye wakaazi wengi, pamoja na mji mkuu, Manila.