Raia wa Ufaransa atekwa nyara Mali

Raia wa Ufaransa atekwa nyara Mali
Image caption Raia wa Ufaransa atekwa nyara Mali

Ufaransa imethibitisha kuwa raia wake mmoja katika shirika la msaada, ametekwa nyara kaskazini mwa Mali.

Wizara ya mashauri ya nchi za nje inasema, Sophie Petronin, alitekwa mjini Gao, kaskazini mwa nchi.

Imesema amekuwa akilifanyia kazi shirika la kuwasiadia watoto wanaougua utapia mlo.

Hakuna kundi lilodai kumteka msaidizi huyo.