Misri yamkamata mwanahabari wa Al-Jazeera

Shirika la habari la Al-jazeera Haki miliki ya picha AFP
Image caption Shirika la habari la Al-jazeera

Serikali ya Misri imedhibitisha kwamba inamzuilia mwanahabari kutoka shirika la habari la AlJazeera aliyekamatwa Ijumaa.

Wizara ya usalama wa ndani inasema mwanahabari huyo, Mahmoud Hussein, atazuiliwa kwa kipindi cha siku 15 kwa tuhuma za kuchochea maasi na kusambaza habari za uongo.

Al Jazeera imepigwa marufuku ya kuendesha shughuli zake nchini Misri, na imelaani hatua hiyo.

Kulingana na Aljazeera, mwanahabari huyo raia wa Misri alikuwa nchini humo likizoni.

Aljazeera inahofia usalama wa mwanahabari huyo.