Israel yaishutumu Marekani kwa kupanga kura dhidi yake

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Waziri mkuu wa Israeli amefanya kikao na balozi wa Marekani nchini humo baada ya kuamuru afike mbele yake kueleza kwa nini Marekani ilipitisha mswada wa mazungumzo katika Umoja wa Mataifa wa kuikosoa Israeli.

Maelezo zaidi kuhusu mkutano huo hayajatolewa.

Hatua hiyo inajiri baada ya Israel kuwaita mabalozi wa mataifa mengine ambao waliunga mkono kura hiyo dhidi ya Israel.

Netanyahu: Israel haitaheshimu azimio la UN

Ban Ki-moon akosoa pendekezo la Netanyahu

Israel yawashtumu mabalozi wa UK, Urusi, China na Uhispania

Mkutano huo unajiri baada ya Israel kuapa kuchukua hatua za kulipiza kisasi kwa kile ilichokitaja kuwa ''hatua ya aibu'' iliochukuliwa na Marekani.

Hatua hiyo ambayo imekosoa ujenzi wa Israel katika eneo la West Bank na Jerusalem ilipitishwa baada ya Marekani kutoshiriki katika kura hiyo badala ya kutumia uwezo wake wa kuipinga.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa uliokosoa mpango wa Israel kutekeleza ujenzi katika maeneo ya Palestina

Israel imeishutumu Marekani ,ambaye ni mshirika wake wa karibu na mkosoaji wa ujenzi wa makaazi katika eneo la Palestina kwa kuanzisha kura hiyo -swala ambalo Marekani imekana.

''Kutokana na habari tulizonazo ,hatuna wasiwasi kwamba serikali ya Obama ilishinikiza kura hiyo ikashiriki pakubwa na kutaka ipitishwe'', alisema waziri mkuu Benjamin Netanyahu.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii