Wapinga sheria ya mapenzi ya jinsia moja Taiwan

Maandamano ya kupinga mapenzi ya jinsia moja yafanyika Taiwan
Image caption Maandamano ya kupinga mapenzi ya jinsia moja yafanyika Taiwan

Maelfu ya raia wa Taiwan kutoka makundi yaliyo na misimamo tofauti wanaandamana nje ya bunge la taifa hilo wakati ambapo kamati ya bunge inatathmini mapendekezo ya kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja.

Waandamanaji wanaopinga mswada huo wa sheria wanapiga kelele wakisema 'ndoa yafaa kuamuliwa na kila mtu', 'andaeni kura ya maoni'.

Kulitokea mfarakano baina ya polisi na waandamanaji, waliokuwa na nia ya kuingia ndani ya bunge kusambaratisha shughuli za kamati ya bunge inayotathmini mswada huo wa sheria.

Wapinzani, wengi wakitoka kwenye makundi ya kidini wanasema kuhalalisha ndoa za jinsia moja kutasambaratisha msingi wa familia, shule zitaanza kutoa mafunzo ya jinsia moja, na pia wanafunzi huenda wakajaribu kuwa wapenzi wa jinsia moja.

Iwapo sheria hiyo itapitishwa, Taiwan itakuwa taifa la kwanza bara Asia kuidhinisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja.

Mirengo yote ya kisiasa inaunga mkono sheria hiyo, japo kura ya maoni imebaini kwamba raia wanatofautiana kimawazo.