Ni vipi Smartphone ilijipatia umaarufu

simu ya iPhone Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ni dhahiri kwamba iPhone ni kifaa chenye faida ya pesa isiyo na kifani

Tarehe 9 Januari 2007,mmoja wa wajasiliamali wenye umaarufu mkubwa katika sayari dunia alitangaza kitu kipya - bidhaa ambayo ilikuwa na faida kubwa zaidi katika historia.

Bila shaka ulikuwa ni uvumbuzi wa iPhone. Kuna njia nyingi ambazo iPhone imeweza kubadilisha mtizamo katika uchumi wa kisasa.

Ni kitu chenye faida isiyo na kifani, kusema ukweli: Kuna makampuni mawili ama matatu yanayopata faida ya pesa nyingi duniani kama kama Apple ambayo hutengenezwa na iPhone pekee.

Ukweli ni kwamba ilitengeneza aina mpya ya bidhaa ambayo ni smartphone.

iPhone na wanaotengeneza bidhaa zinazofanana huwakilisha bidhaa ambayo haIjawahi kuwepo duniani miaka 10 iliyopita lakini kwa sasa ni kitu ambacho kinapendelewa na binadamu wengi. Kuna njia ambayo iPhone imebadilisha masoko mengine - software, muziki na hata matangazo ya biashara.

Lakini haya ni maelezo ya kweli ya awali tu kuhusu iPhone.

Na ukichunguza kwa kina zaidi, msururu wa mafanikio yake ni wa kushangaza. Tunampa sifa zote Steve Jobs na viongozi wengine katika kampuni ya Apple -mshirika wake wa karibu Steve Wozniak, mrithi wake Tim Cook, muundandaji wa mitindo ya iPhone Sir Jony Ive - hata hivyo wahusika muhimu katika historia hii wamesahaulika.

Image caption Miongoni mwa vitu vilivyoifana Smartphone kupendwa ni muundo wake wenye mvuto, uwezo wa mtumiaji kutumia kurasa mbali mbali kwa wakati mmoja

Mambo yaliyoyojiokeza kwa uvumbuzi wa uchumi wa kisasa , kimawazo na ugunduzi yaliyosaidia kuunda uchumi wa dunia tunamoishi.

Ni Idhaa ya dunia ya BBC . Inaweza kuisikiliza mtandaoni ama kujisajili kupokea kipindi kupitia podcast.

Jiulize mwenyewe : ni nini hasa kubachoifanya iPhone kuwa iPhone? Ni muundo wake wenye mvuto, uwezo wa mtumiaji kutumia kurasa mbali mbali kwa wakati mmoja, namna software yake inavyofanya kazi na hardware .

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mtengenezaji wa mtindo wa Apple Sir Jony Ive (kati kati) amesifiwa na wengi kwa mchango wake katika mafanikio ya iPhone

Ubunifu wa kuvutia wa ndani ya iPhone ni baadhi ya vitu muhimu ambavyo imeweza kuvifanya, na smart phones nyingine.

Mwanauchumi Mariana Mazzucato ameotoa orodha ya baadhi ya vitu muhimu ambavyo vinaiwezesha teknolojia ya smartphone kufanya kazi : 1) ubora wa kuimarishwa kwa kasi, 2)uwezo wa kuhifadhi mambo, 3) ubora wa hard drives pamoja na 5)batri zenye nguvu .Huo ni upande wa hardware.

Pia kuna upande wa mitandao na software. Kwa hiyo 6) uwezo wake wa haraka wa kubadili mahesabu madogo ya haraka yanayoiwezesha kubadili mawimbi ya analogi kama vile sauti na mwangaza pamoja na mawimbi ya radio katika mfumo wa dijitali ambayo komputa inaweza kuyamudu.