Waziri mkuu wa Japan, kutembelea bandari ya Pearl

Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe Haki miliki ya picha AP
Image caption Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe

Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe amewasili Hawaii, miaka 75 baada ya Japan kuishambulia bandari ya Pearl na kusababisha Marekani kuingia katika Vita kuu ya Pili ya Dunia.

Kabla ya kuondoka Japan, Waziri Mkuu Abe alituma ujumbe kwamba Japan kamwe haitorudia ukatili wa kivita, iliyofanya awali.

Anatarajiwa kushiriki katika kumbukumbu hiyo, pamoja na Rais Barack Obama wa Marekani, ambaye ataadhimisha kwa kutoa heshima kwa mabaharia na askari maji elfu mbili na mia nne, waliouawa katika shambulio hilo la mwaka 1941.

Hata hivyo Waziri mkuu wa Japan hatarajiwi kuomba msamaha, lakini ataelezea masikitiko yake kufuatia shambulio hilo, kama alivyofanya Rais Obama, Mwezi Mei wakati alipotembelea mji wa Hiroshima, ambapo Marekani ili ushambulia mji huo kwa bomu la kwanza la Nyuklia mwaka 1945.