Gavana aliyetusi Quran afunguliwa mashtaka

Basuki Tjahaja Purnama ni gavana wa Jakarta anayekabiliwa na mashtaka ya kuitusi Quran nchini Indonesia
Image caption Basuki Tjahaja Purnama ni gavana wa Jakarta anayekabiliwa na mashtaka ya kuitusi Quran nchini Indonesia

Mahakama nchini Indonesia imeruhusu kesi dhidi ya gavana wa Jakarta ambaye ni mkristo, kwa mashtaka ya kutusi Quran.

Kesi hiyo inaonekana kupima uhuru wa kuabudu katika taifa hilo lenye waislamu wengi.

Mawakili wanaomtetea Basuki Tjahaja Purnama walitaka kesi hiyo itupiliwe mbali, wakidai kuwa mashtaka hayo yanakiuka haki za kibinaadamu mbali na utaratibu wa kikatiba unaolinda haki za walio wachache.

Kesi hiyo inatarajiwa kusikizwa mapema mwezi ujao.

Iwapo atapatikana na hatia, bw Purnama huenda akahudumia hadi miaka mitano jela.

Indonesia ina sheria kali za kukufuru duniani.