Jina la Fidel Castro, kutotumika katika majengo na mitaa

Fidel Castro Haki miliki ya picha Others
Image caption Fidel Castro

Bunge la Cuba limepitisha kwa kauli moja katazo la kuzuia majengo, mitaa au minara ya kumbukumbu kupewa jina la mwanamapinduzi mkongwe nchini humo Fidel Castro, ambaye alifariki dunia mwezi uliopita.

Rais wa Cuba Raul Castro amesa kaka yake alipinga mitindo hiyo na hadi kufikia hatua ya kuliwasilisha suala hilo bungeni kupigiwa kura.

Fidel Castro aliongoza mapinduzi ya Cuba, ambayo mwaka 1959, waliuondoa madarakani utawala uliokuwa ukiungwa mkono na Marekani.

Aliifanya nchi hiyo kuwa ya Kikomunisti na kubaki kwenye utawala kwa takriban miongo mitano.