Wachina 3 washtakiwa Marekani kwa udukuzi

Waendesha mashtaka mjini New York wamewashtaki raia watatu wa China kwa tuhuma za udukuzi wa mitandaoni
Image caption Waendesha mashtaka mjini New York wamewashtaki raia watatu wa China kwa tuhuma za udukuzi wa mitandaoni

Waendesha mashtaka mjini New York wamewashtaki raia watatu wa China kwa tuhuma za udukuzi wa mitandaoni.

Wanadaiwa kudukua kompyuta za ofisi binafsi za wanasheria wa Marekani wanaotoa ushauri kuhusu kuhusu ubia wa kibiashara.

Wadukuzi hao wanasemekana waliiba taarifa muhimu ambazo ziliwafaidi pakubwa pale waliozitumia kununua hisa baada ya kupata habari za ndani za kampuni walizolenga.

Mmoja wa wadukuzi hao alikamatwa Hong Kong, huku wengine wakiwa wangali wanasakwa.

Kwa upande wake kampuni zimeshauriwa kuchukua hatua zaidi za kulinda taarifa zao za siri kuhusu biashara na kazi zao.