Samir Nasri akana kuzozana na mpenziwe mtandaoni

Samir Nasri
Image caption Samir Nasri

Mvutano wa kiungo wa Ufaransa anayeichezea klabu ya Sevilla ya Uhispania, Samir Nasri, na mchumba wake wa zamani Anatra Antanes umechukua mkondo mpya, baada ya mtandao rasmi wa Twitter wa Nasri kuchapisha maandishi yaliyodokeza udanganyifu uliojiri kati yao na kuhusisha hospitali moja nchini Uhispania.

Ukurasa huo ulisema alipokea huduma ya kimapenzi kutoka kwa madaktari alipokuwa akiuguza jeraha.

Hata hivyo Nasri ameomba msamaha kwenye akaunti yake ya Twitter na kupinga maandishi hayo. ''Akaunti yangu ilidukuliwa, mniwie radhi kwa yaliyotendekea, aliandika,''.

Machapisho hayo yalifichua kuwa mpenzi wake wa zamani, Anara Antanes aliandaa huduma hiyo. Nasri aliwahi kulaumiwa kuwa na udanganyifu na kufanya uhusiana nje ya mapenzi yake na Anara.

"Poleni, nilihitajika kuwaambia kuwa mchumba wangu, Anara aliyekuwa nami wakati huo, alimleta msichana huyo kunipa dawa. "alipowasili, Anara aliondoka chumbani na msichana huyu akaulizia nambari yangu ili kutoka nami usiku huo.

Maandishi hayo yalimkasirisha Antanes, ambaye aliandika kwenye Instagram kuwa, "Pia wewe unatoa huduma ya kimapenzi".

Ingawa maandishi hayo yaliondolewa baadaye, yalifuatwa na maandishi yaliyopinga kuondolewa kwao. Yote niliyosema ni ukweli asilimia 100. Msichana huyo alikuja chumbani kwangu saa tisa usiku na kutoa huduma zisizopo kwenye menyu yao.

Nasri ambaye aliiwakilisha Arsenal kabla ya kujiunga na Manchester City, amekuwa na wakati mgumu mwanzoni mwa msimu huu, baada ya kocha mpya, Pep Guardiola, kudai kuwa amenenepa.

Hatua hiyo ilmfanya kiungo huyo kujiunga na Sevilla kwa njia ya mkopo.