Israel yasitisha kura ya ujenzi katika maeneo ya Palestina

Ujenzi wa makaazi katika maeneo yanayokaliwa na Israel huko Palestina Haki miliki ya picha EPA
Image caption Ujenzi wa makaazi katika maeneo yanayokaliwa na Israel huko Palestina

Kamati kuu ya manispaa ya mji wa Jerusalem nchini Israel, imeahirisha mipango ya kupiga kura ya uidhinishaji wa ujenzi wa nyumba mpya zaidi ya 500 kwa Waisraeli, mashariki mwa mji huo.

Hatua hiyo inakuja siku kadhaa baada ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuitaka Israeli kukomesha mara moja ujenzi wa makao kwa walowezi wa kiyahudi katika ardhi ya Palestina.

Image caption Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Mwanachama mmoja wa kamati hiyo ameiambia BBC kuwa, uamuzi huo umechukuliwa baada ya ofisi ya waziri mkuu kuiandikia kamati hiyo barua, ikisema kuwa ujenzi huo utazidisha zaidi uhasama kati ya Washington, kabla ya kufanyika kwa hotuba maalum kutoka waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani John Kerry, kuhusu kukwama kwa mazungumzo ya amani mashariki ya kati.