Donald Trump aiambia Israel ''kukaa imara''

Rais mteule wa Marekani Donald Trump
Image caption Rais mteule wa Marekani Donald Trump

Rais mteule wa Marekani ameiambia Israel kukaa imara hadi pale atakapochukua mamlaka mwezi ujao.

Pia amesema kuwa Israel imekosewa heshima na kwamba hilo lazima lisitishwe.

Ni matamshi yake ya hivi karibuni katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

Trump: UN ni baraza la porojo

Israel yaishutumu Marekani kwa kupanga kura dhidi yake

Netanyahu: Israel haitaheshimu azimio la UN

Wakosoaji wamemwambia rais huyo mteule kutumia njia rasmi za kuwasiliana kuhusu maswala ya kimataifa.

Siku ya Ijumaa, Marekani iliamua kutoshiriki katika kura ya vetoe kuhusu uamuzi wa Umoja wa Mataifa unaokataza Israel kuendeleza ujenzi wa makaazi katika maeneo ya Palestina inayokalia.

Image caption Makaazi ya wayahudi katika maeneo yanayokaliwa na Israel nchini Palestina

Katika machapisho ya mtandao wa Twitter siku ya Jumatano mjini New York, Bw Trump alisema: Hatuwezi kuruhusu Israel kutoheshimiwa.Marekani ilikuwa rafiki mkubwa wa Israel ,lakini sio tena. Mwanzo wa kumalizika kwa urafiki huo ni pale Marekani ilipokubali kuingia katika makubaliano na Iran, na sasa Umoja wa Mataifa ! Kaa imara Israel,tarehe 20 mwezi Januari inakaribia!

Zaidi ya Wayahudi 500,000 wanaishi katika makao 140 yaliojengwa na Israel tangu uvamizi wake 1967 ambapo walikalia maeneo ya West Bank na mashariki mwa Jerusalem.

Makaazi hayo sio halali kulingana na sheria ya kimataifa ,ijapokuwa Israel inapinga hilo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii