Sheria ya uchaguzi Kenya: Maseneta waafikiana

Bunge la seneti nchini Kenya lataka mjadala wa uma kufanywa kuhusu sheria ya uchaguzi
Image caption Bunge la seneti nchini Kenya lataka mjadala wa uma kufanywa kuhusu sheria ya uchaguzi

Bunge la Kenya limeagiza kufanyika kwa mjadala wa umma kuhusu mabadiliko ya sheria ya uchaguzi yanayoruhusu matumizi ya njia mbadala isiyokuwa ya kielektroniki katika uchaguzi mkuu ujao mwakani.

Katika kikao maalum cha bunge la seneti, spika wa bunge la seneti bwana Ekwe Ethuro aliagiza kamati maalum inayoshughulikia maswala ya kikatiba kujumuisha maoni ya washika dau wote kabla ya swala hilo kujadiliwa upya katika bunge hilo.

Kikao hicho kilifanyika huku muungano wa upinzani ukielekea mahakamani kupinga uhalali wa vikao hivyo maalum vya mabunge yote mawili.

Mabadiliko hayo yaliibua hasira miongoni mwa vyama vya upinzani vikidai kuwa ni njama ya kuiba kura.

kikao maalum cha bunge la seneti la Kenya ,,,,kilianza kwa cheche kali maseneta wakipinga vikali kuwepo kwa idadi kubwa ya maafisa wa polisi nje ya bunge,,,,

Kisa na maana ,,,,,,,,macho ya wakenya wote yalikuwa yakitazama Bunge hilo baada ya spika wa senetibw Ekwee Ethuro kuitisha kikao maalum ilikujadili hatua ya bunge la taifa kupitisha mswada wa marekebisho ya sheria ya uchaguzi ilikuruhusu matumizi ya njia mbadala ya mfumo wa daftari na sajili ya wapiga kura endapo njia ya kielektroniki itafeli katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwakani.

Kulinagana na mwandishi wa BBC Idris Situma hali ilitarajiwa kuwa ngumu kwa upande wa upinzani kulishawishi bunge hilo na upande wa serikali kufutilia mbali sheria hiyo, kwani muungano wa Jubilee uko na jumla ya maseneta 25 huku upinzani ukiwa na wajumbe 22.

Kinyume na matarajio ya wengi, wajumbe wa upinzani na wale wa serikali walikubaliana kwa sauti moja kuwa kulikuwa na haja ya kutafuta uwiano.

Na baada ya cheche kali za maneno, hatimaye spika wa bunge hilo alishawishika na kutoa kauli hii iliyowafurahisha sana pande zote hizo.

Mabadiliko hayo yaliyopitishwa na bunge la taifa juma lililopita yaliibua hasira miongoni mwa vyama vya upinzani nchini Kenya kwa hofu kuwa yangewezesha wizi wa kura katika uchaguzi mkuu ujao.

Wajumbe wa pande zote walimlimbikizia sifa na pongezi spika wa bunge la seneti wakimtaja kuwa hodari na mwenye busara, kwani kauli ya bunge la taifa ilikuwa imeibua taharuki nchini huku vyama vya upinzani chini ya vuguvugu la NASA vikiitishia maandamano kuanzia tarehe 4 mwakani.

Muungano wa upinzani Cord tayari umekwenda mahakamani kupinga vikao maalum vya mabunge yote mawili ukihoji uhalali wake.

Cord vilevile inadai kuwa viongozi wa mabunge hayo mawili walikiuka katiba ya taifa kwa kuwazuia raia na waandishi wa habari kuhudhuria vikao hivyo.