Netanyahu aipinga hotuba ya Kerry kuhusu makaazi

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Image caption Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, ameshutumu hotuba ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani , John Kerry, akidai inaikosoa Israel kimaonevu.

Netanyahu anasema Bw Kerry amekuwa akikosoa saanaa mpango wa Israel wa kupanua maakazi yao katika ardhi ya Palestinian lakini hakosoi vya kutosha uchochezi unaofanywa na Wapalestina.

John Kerry ameutetea uamuzi wa nchi yake wa kuliwezesha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuupitisha uamuzi wa wiki iliyopita, kutangaza makazi ya Wayahudi katika ardhi ya Wapalestina kuwa ni kitendo kinachokiuka sheria za kimataifa.

Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry

Kerry amesema hatua hiyo ina nia ya kulinda uamuzi wa kuwepo kwa mataifa mawili ili kuzuia hatari ambayo ingeweza kutokea.

Amesema bila ya usalama wa Israel na uwepo wa Palestina, Israel hakutakuwa na amani kamili.

Lakini hata hivyo, Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameelezea kuvunjwa moyo na hotuba hiyo, ambayo ameielezea kuwa sio sawa.

Image caption Makaazi ya Israel nchini Palestina

Amesema ukweli ni kwamba Wapalestina wamekataa kukubali uwepo wa Israel.

Kwa upande wake, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amesema atakuwa tayari kurudi katika mazungumzo pale tu Israel itakapoacha kujenga makaazi mapya ya wananchi wake katika eneo la Wapalestina.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii