Afariki dunia, siku moja baada ya kifo cha binti yake

Debbie Reynolds na binti yake Carrie Fisher Haki miliki ya picha AP
Image caption Debbie Reynolds na binti yake Carrie Fisher

Msanii wa Hollywood Debbie Reynolds amefariki akiwa na umri wa miaka 84, siku moja tu baada ya kifo cha binti yake, Carrie Fisher.

Alikimbizwa hospital baada ya kushikwa na ugonjwa nyumbani kwa mtoto wake wa kume huko Beverly Hills.

Debbie Renolds ama Mary Frances, umaarufu wake ulikuwa mwaka 52, wakati alipofanya tamasha sambamba na Gene Kelly katika wimbo uliojulikana kama ''..Singin' in the Rain..''

Alikuwa pia ni muigizaji wa sanaa ya vichekesho