Putin: Serikali na waasi wakubaliana kusitisha vita Syria

Serikali ya Syria yakubaliana na waasi kusitisha vita Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Serikali ya Syria yakubaliana na waasi kusitisha vita

Serikali ya Syria na makundi ya waasi wamekubaliana kusitisha vita na kuanza mazungumzo ya amani ,kulingana na rais wa Urusi Vladmir Putin.

Hatua hiyo inatarajiwa kuanza usiku wa manane Alhamisi.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Uturuki Mevlut Cavusoglu alisema awali kwamba Uturuki na Urusi watakuwa mashahidi katika mpango huo.

Mataifa hayo mawili yanaunga mkono makundi pinzani katika mgogoro huo ambao umeendelea kwa zaidi ya miaka mitano.

Makubaliano hayo hatahivyo hayashirikishi makundi mawili ya Jihad nchini Syria ,likiwemo kundi la Islamic State na Jabhat Fateh al- sham ambalo lilijulikana kama Nusra Front .

Image caption Ramani ya Syria

Lakini yanashirikisha eneo linalodhibitiwa na waasi la mashariki mwa Ghouta karibu na Damascus ambalo limeorodheshwa kuwa eneo muhimu katika mazungumzo hayo.

Mapema mwezi huu, Moscow na Ankara walijadiliana kuhusu usitishwaji wa vita katika mji mkuu wa pili kwa ukubwa nchini Syria, Aleppo ambayo yalisababisha maelfu ya waasi na raia kuondoshwa katika eneo lililokuwa limezingirwa na vikosi vya serikali.

Makubaliano mengine ya kusitisha vita yalioafikiwa kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa, Marekani au Urusi yameshindwa kuafikiwa.