Klabu ya China kumlipa Tevez zaidi ya pauni 310,000 kwa wiki

Shenghai wamemsajili mshambuliaji huo mwenye umri wa miaka 32, kutoka klabu ya Boca Juniors Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Shenghai wamemsajili mshambuliaji huo mwenye umri wa miaka 32, kutoka klabu ya Boca Juniors

Aliyekuwa mshambuliaji wa kalabu ya Manchester City Carlos Tevez amejiunga na klabu ya China Shenghai Shenhua ,klabu hiyo imethibitisha.

Shenghai wamemsajili mshambuliaji huo mwenye umri wa miaka 32, kutoka klabu ya Boca Juniors lakini hakuna maelezo yaliotolewa kuhusu kandarasi hiyo.

Shanghai inayofunzwa na Gus Poyet imeripotiwa kuweka kandarasi ya pauni milioni 40 ikiwemo mshahara wa zaidi ya pauni 310,000 kwa wiki.

Boca Juniors imesema: Kila la kheri Carlitos. Utakuwa myoyoni mwetu kila wakati.

Tevez alicheza kwa miaka saba katika ligi ya Uingereza na akajishindia mataji ya ligi akiwa na timu zote mbili za Manchester.

Pia alishinda taji la vilabu bingwa Ulaya akiwa na United mwaka 2008 kabla ya kujiunga na Juventus mwaka 2013, ambapo alijishindia mataji mawili ya ligi ya Itali.

Mnamo tarehe 23 mwezi Disemba Chelsea iliingia katika mkataba na Shanghai kumnununua kiungo wa kati wa Chelsea Oscar katika uhamisho utakaogharimu pauni milioni 60.