Aliyepanga shambulio kwenye daraja mjini Lagos mbaroni

Daraja la Lagos Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Daraja hili linaunganisha wilaya ya kati yenye shughuli za kibiashara mjini Lagos-iliyoko kwenye kisiwa na maeneo mengine ya mji huo

Polisi nchini Nigeria wanasema kuwa wamemkamata kiongozi wa genge lililokuwa linapanga kulipua daraja kubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Lagos.

Maafisa wanasema pia wamebaini vilipuzi na vifaa vya kulipua mabomu pamaoja na silaha wakati wa uchunguzi.

Polisi imedai mshukiwa alikuwa kiongozi wa kundi la wapiganaji na mtaalam wa vilipuzi.

Mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 43 anadaiwa kupanga kulipua daraja tatu nchini humo.

Daraja hilo linaunganisha wilaya ya kati yenye shughuli za kibiashara mjini Lagos-iliyoko kwenye kisiwa na maeneo mengine ya mji huo.

Police wanasema wanawasaka wajumbe wengine wa genge hilo.

Afisa mmoja amesema kuwa mshukiwa alikuwa na uhusiano na kundi la wanamgambo wanaoendesha harakati zao katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta.

Jimbo hilo limekumbwa na mashambulio ambayo yamesababisha kugawanyika kwa kugawanyika kwa uzalizaji wa mafuta kwa kiango ya asilimia tatu.