Walipakodi wa Uganda watalipa kodi yao kupitia Benki ya Kenya KCB

Mkurugenzi mkuu wa KCB Joshua Oigara Haki miliki ya picha The EastAfrican
Image caption Mnamo tarehe 21 mwezi huu, KCB ilipigwa marufuku na mamlaka ya kwamba ikukiuka sheria za malipo ya ushuru

Mamlaka ya Ushuru nchini Uganda (URA) imetoa ruhusa kwa benki inayomilikiwa na Kenya, KCB kutumika kulipia kodi na raia wa taifa hilo.

Hii ni baada ya Mamlaka hiyo kuzuia matumizi ya benki hiyo kutokana na mzozo ulioibuka kufuatia kesi iliyowahusu wateja wa benki hiyo na mamlaka hiyo ya Ushuru.

Mnamo tarehe 21 mwezi huu, KCB ilipigwa marufuku na mamlaka hiyo kwa kukiuka sheria za malipo ya ushuru.

Kupitia mtandao wake rasmi, mamlaka hiyo emeandika, "Tunawaarifu wananchi walipa ushuru kuwa mamlaka ya ushuru nchini imeirejesha benki ya KCB kwenye mtandao wake. Kwa hivyo tunawahakikishia wateja wetu kuwa masuala yote yamesuluhishwa . Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliofanyika.

Uamuzi huu utawawezesha raia wa Uganda kutumia benki hiyo kulipa ushuru pamoja na huduma nyingine za serikali.

Benki ya KCB pia imethibitisha kuondolewa marufuku hiyo kwa kuwaandikia wateja wake.

"Huduma za malipo ya ushuru kupitia benki ya KCB zimerejea na wateja wetu wanaweza kupokea huduma hizo kupitia matawi ya benki yetu ya KCB nchini Uganda". KCB ilijitetea kuwa iliathirika kutokana na mzozo uliosbabbiushwa na wateja wake na mamlaka ya ushuru.

Benki hiyo yenye makao makuu mjini Nairobi, ni mojawapo ya benki maarufu Afrika Mashariki kwani mbali na Uganda, ina matawi katika mataifa ya Tanzania, Burundi, Sudan Kusini na Rwanda.