Wasichana wafanya vema katika mtihani wa kidato cha 4 Kenya

Matokeo hayo yameonyesha kupungua kwa alama bora ikilinganishwa na miaka ya awali. Ni asilimia 15 tu ya wanafuzi wamefuzu kujiunga na elimu ya chuo kikuu kwa moja.
Image caption Waziri wa elimu nchini Kenya Fred Matiang'i

Zaidi ya wanafunzi laki tano waliofanya mtihani wa Kiwango cha shule ya upili, nchini Kenya wamepokea matokeo yao leo kwa manung'uniko.

Waziri wa Elimu, nchini humo, Fred Matiangi aliyatangaza matokeo hayo mjini Mombasa kinyume na ilivyokuwa awali ambapo mji wa Nairobi ulitumika kufanya shughuli hiyo.

Matokeo hayo yameonyesha kupungua kwa alama bora ikilinganishwa na miaka ya awali. Ni asilimia 15 tu ya wanafuzi wamefuzu kujiunga na elimu ya chuo kikuu kwa moja.

Aidha wasichana walifanya bora katika orodha ya wanafuzi 20 bora nchini humo. Kumi na sita kati yao walikuwa ni wasichana huku wavulana wakiwa ni wanne pekee.

"Shule nyingi zilizokuwa zinaandikisha A nyingi, zimepata mbili pekee," alisema.

Bwana Matiangi aliyebandikwa jina Magufuli, baada ya Rais wa Tanzania John Magufuli, alisema kupungua kwa matokeo bora ilikuwa ni mafaniko ya kuziba nyufa za wizi wa mtihani.

Hata hivyo, hakuna kisa chochote cha udanganyifu kilichoripotiwa.

Wakati huo huo, Rais Uhuru Kenyatta ametoa agizo la kuondolewa kwa nambari ya mtihani kuwatambulisha wanafunzi na kubadilishwa na nambari ya siri.

Taifa hilo lilikumbwa na wimbi la kuteketezwa kwa mabweni na wanafunzi baad aya sheria kali za kuzuia wizi wa mtihani kufanikishwa na waziri huyo.