Netanyahu akana kashfa ya ufisadi inayomkabili

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekana kuhusika katika ufisadi wa aiana yoyote
Image caption Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekana kuhusika katika ufisadi wa aiana yoyote

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekana kufanya makosa yoyote kufuatia madai ya ufisadi yanayomkabili katika vyombo vya habari.

Kumekuwa na madai kwamba alipokea zawadi kinyume na sheria kutoka kwa wafanyibiashara, na kwamba mwanasheria mkuu wa taifa hilo anatarajiwa kuanzisha uchunguzi.

Lakini katika taarifa yake Netanyahu amesema kuwa uchunguzi huo utafeli kupata ushahidi wowote dhidi yake.

Amesema kuwa hakuna chochote cha kuficha.