Al-Nusra front: Hatutasitisha vita Syria

Wapiganaji wa kundi la Al- Nusra Front
Image caption Wapiganaji wa kundi la Al- Nusra Front

Kundi moja la waasi ambalo awali lilijulikana kama Al-Nusra Front limessema haliutambui mkataba wa sasa wa kusitisha vita vya Syria.

Kundi hilo lililokuwa na uhusiano na Al Qaeda limesema litaendelea na mapambano yake dhidi ya utawala wa rais Bashar al-Assad.

Kundi hilo ni mojawapo ya yale makundi ya wapiganaji ambayo hayakushirikishwa kwenye makubaliano hayo ya usitishwaji wa mapigano yaliyoanzwa kutekelezwa hapo jana.

Kwa sasa vita vimesitishwa katika maeneo mengi nchini Syria isipokuwa visa vichache tu vilivyoripotiwa.

Urusi na Uturuki waliohusika katika duru hii ya makubaliano wamesema wanatumai baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litaidhinisha makubaliano hayo hii leo.

Mada zinazohusiana