Angela Merkel: Ugaidi ni tishio kubwa Ujerumani

Chansela wa Ujerumani Angela Marekel amesema kuwa ugaidi ndio changamoto kuu Ujerumani
Image caption Chansela wa Ujerumani Angela Marekel amesema kuwa ugaidi ndio changamoto kuu Ujerumani

Chansela wa Ujerumani Angela Merkel, amesema tatizo la ugaidi ndio changamoto kubwa kwa taifa lake.

Ameyasema hayo katika ujumbe wake wa mwaka mpya.

Bi Merkel, alitaja mfano wa lile shambulio ambapo dereva mmoja Mtunisia aliwagonga watu kwa makusudi na kusababisha vifo vya watu 11 mapema mwezi huu huko Berlin.

Amesema haieleweki ni vipi mtu anayetafuta hifadhi Ujerumani anaweza kuja kuwashambulia Wajerumani.

Hata hivyo ameonya dhidi ya kueneza chuki kwa kundi zima la watu kwa sababu ya vitendo vya wachache miongoni mwao.

Mada zinazohusiana