Trump ampongeza Putin kwa kutolipiza kisasi

Rais Putin wa Urusi na rais mteule wa Marekani Donald Trump
Image caption Rais Putin wa Urusi na rais mteule wa Marekani Donald Trump

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amempongeza mwenzake wa Urusi Vladmir Putin kwa kutowafukuza wanadiplomasia wa Marekani ,licha ya Marekani kufanya hivyo kujibu madai ya kuingilia uchaguzi wa Marekani.

Bwana Trump alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter: Hatua nzuri ya kusubiri, nilijua kwamba yeye ni mwerevu sana!.

Israel yaishutumu Marekani kwa kupanga kura dhidi yake

Donald Trump aiambia Israel ''kukaa imara''

Natenyahu aipinga hotuba ya Kerry kuhusu makaazi

Moscow imekana madai yoyote ya kuingilia uchaguzi wa Marekani kupitia udukuzi.

Lakini katika hatua moja ya mwisho ya uongozi wa rais Obama ,Marekani iliagiza kuondoka kwa wanadiplomasia 35 wa Urusi kufikia siku ya Jumapili mchana.

Lakini Putin alikataa kulipiza kisasi.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Ujumbe wa Twitter ulioandikwa na Trump akimsifu Putin

Mvutano huo unafuatia madai kwamba Urusi ilidukua kampeni ya chama cha Democrat na mgombea wake Hillary Clinton na kutoa habari kupitia mtandao wa Wikileaks ili kumsaidia Bwana Trump kushinda uchaguzi .

Mashirika kadhaa ya Marekani ikiwemo lile la FBI na CIA yamesema hayo yalitendeka ,lakini Trump amekuwa akipuuzilia mbali madai hayo akisema ni ya ''ujinga''.

Hatahivyo amesema kuwa atakutana na maafisa wa ujasusi nchini Marekani ili kuelezewa hali halisi.

Serikali ya Obama ilitangaza kisasi hicho siku ya Alhamisi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii