Afrika kwa picha 2016

Picha zilizovutia vichwa vya habari barani Afrika mwaka huu:

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Oscar Pistorius alivua miguu yake bandia na kuguchuia katika mahakama wakati wa kusikizwa kwa kesi yake nchini Afrika Kusini
Haki miliki ya picha Wanamaji wa Itali
Image caption Boti iliokuwa ikizama katika bahari ya Mediterenean kati ya Itali na Libya yapigwa picha .Kikosi cha wanamaji wa Italy kiliwaokoa zaidi ya wahamiaji 560.
Haki miliki ya picha AP
Image caption Miezi michache baadaye mnamo mwezi Agosti boti ndo ziliokolewa mojawapo ikiwa mtu na mwanawe wa miaka mitano
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waandamanaji nchini Zimbabwe wazichoma noti za taifa hilo zilizozinduliwa ili kukabiliana na upungufu wa dola za Marekani nchini humo
Haki miliki ya picha AP
Image caption Mnamo mwezo Oktoba wanawake 21 na wasichana waliunganishwa tena na familia zao .Kampeni ya bringbackourgirls iliwafanya kuwa maarufu duniani
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wachezaji wa lemau wa voliboli nchini Rwanda walisimama na kuimba nyimbo ya taifa lao katika mechi dhidi ya China
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sudan Kusini ni maarufu sana kwa mchezo wa miereka na mnamo mwezi Aprili mashindano ya Miereka yalifanyika kwa mara ya kwanza tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waandamanji walioda kuwepo kwa mabadiliko ya sheria za uchaguzi wakikabiliana na maafisa wa polisi katika eneo la Kibera nchini Kenya.
Haki miliki ya picha Alamy
Image caption Mafuriko nchini Somalia yalisababisha familia nyingi kuhama katika majumba yao
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mnamo mwezi Oktoba mwanajeshi wa Sudan Kusini aonekana akipiga tarumbeta ya pembe ya ngombe katika operesheni ya jeshi
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe asherehekea mwaka wa 92 tangu azaliwe mnamo mwezi Februari
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Katika maandamano ya kupiga ukosefu wa ajira nchini Tunisia ,mtu ambaye hana kazi alijishona mdomo wake ikiwa katika kile kiichotajwa kuwa mgomo wa kutokula mnamo mwezi Januari
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mashabiki wakimuomboleza mwana soka wa Nigeria Stephen Keshi nchini Togo mnamo mwezi Juni
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Nchini Afrika Kusini wanafunzi walifanya mgomo dhidi ya karo ya kiwango cha juu
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Katika harakati za kukabiliana na ulemavu wa ngozi ,shindano la mfalme na malkia wa Albino liliandaliwa mjini Nairobi mwezi Oktoba.