Ban Ki-moon akamilisha muda wake UN

Ban Ki-moon akamilisha muhula wake katika Umoja wa Mataifa ambapo amehudumu kama katibu mkuu
Image caption Ban Ki-moon akamilisha muhula wake katika Umoja wa Mataifa ambapo amehudumu kama katibu mkuu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayestaafu, Ban Ki-moon, ameondoka makao makuu ya Umoja wa Mataifa , kwa mara ya mwisho baada ya muhula wake wa mwongo mzima.

Bwana Ban Ki-moon anamaliza kazi rasmi, mwaka mpya unapoingia.

Alisema atakuwako Medani ya Times mjini New York, kuukaribisha mwaka, na kuadhimisha kumaliza kazi.

Alifanya mzaha kwamba mamilioni ya watu watakuwa wakiangalia wakati akipoteza kibarua chake.

Pahala pake panachukuliwa na waziri mkuu wa zamani wa Ureno, Antonio Guterres.

Bwana Ban anatarajiwa kurudi Korea Kusini, ambako kuna tetesi, kwamba huenda akagombea nafasi ya Rais Park Geun-Hye, ambaye anashtakiwa.